Western Bible College

Katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Miaka Kumi ya Mavuno, Kanisa la Tanzania Assemblies of God liliona hitaji la kuanzisha Chuo cha Biblia cha kuwaandaa watumishi wa kuifikia hususani Kanda ya Magharibi na Injili ya Yesu Kristo.

Kwa kutimiza azma hiyo, Idara ya Elimu TAG ilifanya utaratibu wa kununua kiwanja ekari 120 eneo la Ilolangulu, Tabora kwa ajili ya kujenga Chuo. Mchakato huo ulifanyika kwa ushirikiano baina ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Elimu, Mchungaji Jonas Mkoba na aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Tabora wakati ule, Mchungaji Paul M. Meivukie, pamoja na aliyekuwa Mwangalizi wa Sehemu ya Usungu, Mchungaji Immanuel Dominic.

Kiwanja hicho kilinunuliwa toka kwa familia mbili tofauti na malipo yake yalifanyika tarehe 9/6/2014 mbele ya Wakili Musa Kassim. Kufuatia ununuzi huo, Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Dr. Barnabas Mtokambali, alishauri ujenzi kuanza mara moja. Kamati ya Utendaji ya Idara ya Elimu Taifa walifika Tabora kuunda Kamati ya Ujenzi wa Chuo.

edu38

Mch. Kennedy Lukilo

Mkuu wa chuo wa kwanza
edu39

Jengo la Utawala

Western Bible College
edu40

Bwalo la Chakula

Western Bible College

Ufyekaji wa pori ulianza mwezi Juni mwaka 2017 na ujenzi ulianza rasmi tarehe 22/10/2017. Western Bible College (WBC) ilizinduliwa tarehe 19/1/2018 na Askofu Mkuu Dr. Baranabas Mtokambali. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Agrey Mwanri, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui na mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Mama Queen Mlozi, viongozi mbalimbali wa serikali, wajumbe wa Baraza la Watendaji wa Tanzania Assemblies of God, waangalizi, wachungaji, na washirika wa Tanzania Assemblies of God kutoka makanisa ya jirani na Chuo, wananchi wa vijiji vya Mpenge na Ilolangulu, na sehemu zingine mbalimabli.

Chuo kilianza kutoa mafunzo tarehe 22/1/2018 kukiwa na jumla ya wanafunzi 70. Hivi sasa kuna jumla ya wanafunzi 100. Chuo kina walimu 5, wanne wa muda wote na mmoja wa muda.