Mafunzo ya Uzamili

Kitengo cha mafunzo ya Uzamili katika chuo cha Tanzania Assemblies of God Central Bible College – CBC, Kilizinduliwa tarehe 27 October, 2007 na aliyekuwa Askofu Mkuu wa kipindi hicho Rev. Dr. Ranwell Mwanisongole; kwa sherehe maalumu ya uzinduzi iliyofanyika katika chuo cha Tanzania Assemblies of God (AGBC).

Kitengo hiki kilianzishwa kikiwa chini ya uongozi na utawala wa chuo cha Uzamili cha Nairobi, East Africa Graduate Studies (EAGS), na kilifanya kazi yake kikiwa kivuli cha chuo cha EAGS cha Nairobi chini ya ngazi za utawala: Bodi kuu ya Utawala wa EAGS, ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Missionary Gregory Beggs na wajumbe wa Bodi walikuwa Dr. Chuck Ness (Katibu wa Bodi na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Uzamili – East Africa), Dr Douglas Lowenberg (Makamu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Uzamili – East Africa), Askofu Ranwell Mwanisongole (Mjumbe) na Askofu Njiri (Mjumbe). Mkurugenzi wa elimu Dr. Jotham Mwakimage alikuwa Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Uzamili ya Chuo cha AGBC na Dr. Jackson Nyanda aliyekuwa Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu TAG, alikuwa Makamu Msimamizi Mkuu wa kitengo cha Uzamili cha chuo cha AGBC.

Mkuu wa Chuo cha AGBC wakati huo alikuwa Rev. Ron Swai, alikuwa Mkuu wa Utawala wa uendashaji na Fedha wa kitengo hiki. Dr. Bob Blaswell alikuwa Mwadhili wa Mafunzo campus ya AGBC – Dodoma, na Msajili wa mafunzo ya Uzamili (Registrar) alikuwa Mchungaji Ezekiel Mwakajwangwa.

Darasa la wanafunzi wa kwanza kabisa waliozindua program ya mafunzo ya uzamili katika chuo cha Tanzania Assemblies of God, AGBC Dodoma walikuwa jumla yao kumi na tano (15) na walianza mafunzo ya Uzamili Octoba, 2007.

Kati ya wanafunzi 15 wa kwanza, walofanikiwa kumaliza mafunzo ya Shahada ya Uzamili ni 12 tu. Wanafunzi wawili walikatiza masomo yao mapema kwa sababu binafsi, na mmoja alitwaliwa kwenda kuishi pamoja na Bwana Mbinguni.

Kozi ya kwanza iliyopendekezwa kwa kundi hili la kwanza ni MA Broad Field ambayo ilimuandaa mtu kuwa Mchungaji au Missionary na Kiongozi wa Kiroho. Wanafunzi hawa walihitimu katika mahafali ya November, 2010 na kutunukiwa shahada ya Uzamili (MA Biblical Studies Broad Field) ya chuo Kikuu cha Global (Global University).

Kuanzia mwaka 2013 kulitokea mabadiliko makubwa katika Kitengo cha mafunzo ya Uzamili cha Assemblies of God Bible College Dodoma (AGBC) Kitengo hiki hakikukuwa tena chini ya Chuo cha East Africa Gradute School (EAGS) cha Nairobi, bali kilifanywa kuwa ni kitengo kinachojitegemea, kinachowasiliana na Global University moja kwa moja.

Uongozi huu wa utawala wa Kitengo cha Mafunzo ya Uzamili ni ule ule wa Central Bible College (CBC), na viongozi watendaji ambao wanaunda kamati ya utendaji wa Kitengo cha Mafunzo ya Uzamili ni:

    1. Mchungaji Jonas Petro Mkoba – Mtawala Mkuu wa Fedha (Logistic Officer), Mwenyekiti
    2. Gerald Ole Nguyaine – Mkurugenzi wa Mafunzo ya Uzamili, M/Mwenyekiti
    3. Jackson Ngilu Nyanda, Msajili (Registral), Katibu