Mtama Technical Training Center

Chuo cha Mtama Technical Training Centre (MTTC) kilianza rasimi kutoa huduma ya mafunzo mwaka 2012 kwa fani ya uhazili pekee kikiwa na wanafunzi 12 na chuo kilikuwa hakijasajiriwa, hivyo kiserikari kilikuwa hakijulikana.

Hata hivyo wanafunzi waliondoka kutokana na chuo kutosajiriwa lakini mwaka 2014 tulianza mchakato wa kupata usajiri hatimaye mwaka 2016 walikubali kusajiri chuo kwa fani moja ya uselemara.

Hata baada ya kusajiri chuo tuliruhusiwa kufundisha fani ya useremala pekee kwa sababu imesajiriwa, lakini changamoto yake kulikuwa wanafunzi wa fani hii.

Wakuu wa chuo cha MTTC tangu chuo kilipoanza ni:

  1. Mch Mmari alianza mwaka 2012 – 2013 wakati huo huo alikuwa pia mkuu wa chuo cha Biblia.
  2. Ndugu Benedict Dinho………………………… mwaka 2013 – 2014,
  3. Ndugu James S. Kato…………………………… mwaka 2014 – 2017
  4. Ndugu Mercy F. Swenya………………………… mwaka 2017 hadi sasa.

Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hichi cha mpango mkakati:

Mwaka 2015 chuo cha udereva kilipata usajiri wa kudumu kwa daraja D, na tulianza kufundisha darasa la udereva wa gari na pikipiki. Mwaka 2017 chuo kilipata usajiri wa kudumu chenye namba ya usajiri VET/LND/PR/2016/C/021. Mwaka 2017 tumefanikiwa kuanzisha mradi wa kuku unaojiendesha wenyewe sasa, na mwaka 2018 tulifanikiwa kununua incubator kubwa kwa ajiri ya kutototreshea vifaranga hivyo huo mradi tunauza kuku, mayai na vifaranga. Mwaka 2019 tumefanikiwa kujenga jengo la karakana ya umeme ambayo kwa msaada wa Mungu tunaamini mwakani itaanza rasmi.