Maadili ya Msingi
Idara ya Elimu ya Kanisa la TAG ina maadali ya msingi sita kama yalivyoainishwa hapo chini.
Utakatifu na Uadilifu
Kila mtumishi na mwanafunzi katika Idara ya Elimu atadhihirisha uaminifu wake kwa Mungu kwa kuishi maisha ya utakatifu, uadilifu pamoja na nidhamu ya kiroho katika maeneo yote ya maisha na utumishi wake.
Uaminifu kwa Biblia
Kila mtumishi na mwanafunzi katika Idara ya Elimu ataamini na kudhihirisha kwa matendo na mwenendo wa maisha yake kuwa Maandiko Matakatifu yamevuviwa na Mungu na ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu na ni kiongozi cha imani kisichoshindwa wala kubadilika
Uwajibikaji
Kila mtumishi na mwanafunzi atakuwa wakili mwaminifu kwa kufuata na kutii kanuni na sheria zinazomhusu. Atatakiwa kutumia fedha na mali za Idara kwa kuzingatia taratibu, malengo na makusudi yaliyowekwa. Hii ni pamoja na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha kwa wakati na mahali husika
Kufanya kazi kama timu
Kila mtumishi na mwanafunzi atakuwa na mahusiano yanayoonesha upendo na nia moja inayowezesha kufanya kazi kama timu kwa manufaa ya wote na kwa utukufu wa Mungu.
Ibada
Kila mtumishi na mwanafunzi atadumisha uhusiano wa karibu na Mungu kwa kumsifu, kumwabudu, na kuwa na mawasiliano Naye kwa njia ya kumsikiliza kupitia Neno na maombi.
Ufanisi
Kila mtumishi na mwanafunzi atatimiza wajibu wake kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kupata matokeo bora ya kazi yake.
Uongozi wa Idara ya Elimu TAG

Jonas Mkoba
Mkurugenzi

Gerald Ole-Nguyaine
Makamu Mkurugenzi

Joyce Musembe
Katibu

Tadei Mbuta
Mtunza Hazina

