Fasihi na Theolojia

Kitengo cha Teolojia na Fasihi kilianzishwa chini ya uongozi na utawala wa Idara ya Elimu ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God. Kitengo kilizinduliwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God Dr. Barnabas Weston Mtokambali tarehe 16 Juni 2014 mkoani Morogoro. Kamati ya Idara ya Elimu ilimteua Dr. Jackson Ngilu Nyanda kuwa mwenyekiti, Dr. Immaculate Nhigula kuwa Makamu Mwenyekiti, na Mchungaji George James kuwa katibu wa muda na baadaye aliteuliwa Mchungaji Isaac Challo kuwa katibu wa muda wa kitengo cha Teolojia na Fasihi. Kitengo cha Teolojia na Fasihi ni muungano wa vitengo viwili: kitengo cha Fasihi na Teolojia kuwa kitengo kimoja.

Kitengo cha Teolojia na Fasihi kiliundwa kwa makusudi yafuatayo:

  1. Kujadili mada za Kiteolojia ikiwa ni pamoja na Imani potofu na mafundisho yenye utata. Hii ni pamoja na kufanya utafiti juu ya Imani potofu na kupendekeza fundisho sahihi la Imani ya Kipentekoste.
  2. Kushughulikia mwenendo wa kiteolojia na misimamo ya kiroho ya makundi mbalimbali ndani ya TAG na kuushauri uongozi kitaifa juu wa uamuzi na hatua za kuchukua ikiwa italazimu kutoa tamko la msimamo wa Kanisa au la.
  3. Kusimamia teolojia ndani ya Vyuo vya Biblia kwa kutoa ushauri juu ya mitaala ya vyuo kwa kuzingatia mahitaji ya kanisa la nchi na jamii kwa ujumla.
  4. Kupitia vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa ki-TAG na kupendekeza marekebisho muhimu ya kitafsiri na kufasili kabla ya kuingia sokoni na kusomwa na watu.
  5. Kubuni njia ya kuchochea uandishi wa vitabu kwa walimu wa vyuo vya Biblia na wachungaji wengine wa TAG.
  6. Kutafuta vitabu muhimu na kuvitafsiri kwa manufaa ya kanisa.
  7. Kuchochea uandishi na ushapishaji wa vitabu na majarida mbalimbali yenye maudhui sahihi Kibiblia, Kiteolojia na Imani ya Kipentekoste.

Kamati na Uongozi wa Kitengo cha Teolojia na Fasihi

  1. Dr. Jackson Ngilu Nyanda………………………………………….Mwenyekiti
  2. Dr. Immaculate Nhigula …………………………………………..Makamu Mwenyekiti
  3. Mchungaji Severine Constantine Fusi……………….….……Katibu
  4. Prof. Joseph Amon Kimeme ………………………………….…….Mjumbe
  5. Dr. Ezekiel Mbwilo ……………………………………………………Mjumbe
  6. Mchungaji Agustino Dedu ………………………………………..Mjumbe
  7. Dr. Gerald Ole-Nguyaine ………………………………………….Mjumbe
  8. Mchungaji Elieti Paul Msangi …………………………………..Mjumbe
  9. Dr. Geofrey Peter Majule ………………………………………..Mjumbe
  10.  Mchungaji George James ………………………………………..Mjumbe
  11. Askofu Oral Sossy ……………………………………………………Mjumbe

Pamoja na majukumu yake mengine kitengo hiki pia kinasimamia klabu ya waandishi wa vitabu katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God. Klabu hiyo ilizinduliwa rasmi na Askofu Mkuu wa TAG Dr. Mtokambali tarehe 3 Machi 2017, Central Bible College. Klabu hiyo ina matawi nchi nzima.

Kudhibiti uandishi holela unaopotosha jamii na Kanisa la Mungu ndani ya TAG na Madhehebu mengine. Kitengo kitadhiibiti viwango vya ubora vya uandishi