• KARIBU UJIFUNZE
    IDARA YA ELIMU YA TAG
    Jifunze Uongeze Maarifa
  • Idara ya
    ELIMU
    “Elimu Bora kwa wote”

Kuhusu TAG

Tanzania Assemblies of God (TAG) ilisajiliwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya Societies Ordinance ya mwaka 1954 na kupewa namba ya usajili SO. 6246

soma zaidi

Makao Makuu

Makao makuu ya kanisa pamoja na ofisi ya idara yetu zilihamia Rasmi Dodoma mnamo tarehe 01/11/2021, hivyo huduma zetu zote zinatolewa mkoani Dodoma karibu katika ofisi zetu.

Bezaleli

Kanisa letu lina mfumo wa kidigitali uitwao Bezaleli, ili kuweza kuingia kwenye mfumo wetu tafadhali Bofya Hapa

Kuhusu Idara ya Elimu


Idara ya Elimu ni mojawapo ya Idara kumi na moja za Kanisa la Tanzania Assemblies of God, iliyoanzishwa kwa ajili ya kufanikisha maono na malengo yake. Kusudi la kuwepo kwa Idara ni kupanga, kuratibu, na kusimamia utekelezaji ili kuwa na watumishi waliondaliwa vema kiroho na kitaaluma, wenye kuakisi tabia na mtazamo wa Yesu katika maisha na huduma. Idara inatoa mafunzo kwa watumishi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God na Madhehebu mbalimbali ya Kipentekoste tunayokubaliana nayo kiimani ndani na nje ya nchi.Idara ya Elimu ina Vyuo vya Biblia tisa. Vyuo vya bweni saba, kimoja cha kutwa, na kimoja huria. Ili kuharakisha kazi ya kuivuna Tanzania...

soma zaidi

Lengo letu Kuu


Kuratibu mafunzo yatolewayo katika Vyuo vya Biblia, Vyuo vya Kupanda Makanisa na Mafunzo Endelevu ili kutoa elimu bora kwa lengo la kuwa na watumishi wenye uwezo na maadili ya kibiblia. Kuandaa mtaala wenye sifa zinazohakikisha kwamba elimu inayotolewa inakidhi hitaji la Kanisa la TAG na aina ya cheti kinachotolewa kwa mhitimu.

Shuhuda